Kristo amefufuka kweli Alleluya

SEHEMU YA KWANZA: MASOMO
2 0/ 04/2 025

Somo la Kwanza
Mdo 1 0:34, 37-43
Petro akafumbua kinywa chake, akasema, Jambo lile ninyi mmelijua, lilionea katika Uyahudi wote likianzia Galilaya, baada ya ubatizo aliohubiri Yohane; habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu; naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu aikuwa pamoja naye. Nasi tu mashahidi wa mambo yote yaliyotendeka katika nchi ya Wayahudi na katika Yerusalemu; ambaye walimwua wakamtundika mtini. Huyo Mungu alimfufua siku ya tatu, akamjalia kudhihirika, si kwa watu wote, bali kwa mashahidi waliokuwa wamekwisha kuchaguliwa na Mungu, ndiyo sisi, tuliokula na kunywa naye baada ya ufufuka kwake kutoka kwa wafu. akatuagiza tuwahubiri watu na kushuhudia ya kuwa huyu ndiye aliyeamriwa na Mungu awe mhukumu wa wahai na wafu. Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.

Wimbo wa Katikati
Zab 1 1 8:1 -2, 1 6-1 7, 22-23

Aleluya.
Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema
kwa maana fadhili zake ni za milele.
Israeli na aseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele. (K)
K. Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, Tutashangilia na kuifurahia.

Mkono wa kuume wa Bwana umetukuzwa;
Mkono wa kuume wa Bwana hutenda makuu.
Sitakufa bali nitaishi,
Nami nitayasimulia matendo ya Bwana. (K)
K. Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, Tutashangilia na kuifurahia.

Jiwe walilolikataa waashi
Limekuwa jiwe kuu la Pembeni.
Neno hili limetoka kwa Bwana,
Nalo ni ajabu machoni petu (K)
K. Siku hii ndiyo aliyoifanya Bwana, Tutashangilia na kuifurahia.


Somo la Pili
Kol 3:1 -4
Mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu.

Shangilio
Aleluya
Aleluya Aleluya!
Kristo, Paska wetu amekwisha kutolewa sadaka; Basi natuifanye karamu katika Bwana!
Aleluya

Somo la Injili
Luka 24:1 -1 2
Siku ya kwanza ya juma, alfajiri na mapema, wale wanawake walikwenda kaburini wakileta manukato waliyokuwa wameyatayarisha. Wakalikuta jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, wakaingia ndani lakini hawakuuona mwili wa Bwana Yesu.
Walipokuwa bado wanashangaa juu ya jambo hili, tazama, watu wawili wakiwa wamevaa mavazi yanayong'aa walisimama karibu nao. Wale wanawake wakaingiwa na hofu, wakainamisha nyuso zao chini, lakini wale watu wakawaambia, “Mbona mnamtafuta aliye hai kati ya wafu? Hapo hayupo, amefufuka! Kumbukeni alivyowaambia alipokuwa bado Galilaya: kwamba Mwana wa Adamu hana budi kutiwa mikononi mwa watu waovu, na kusulubiwa, na siku ya tatu kufufuka.”
Wakakumbuka maneno yake, wakarejea kutoka kaburini, wakayatangaza hayo yote kwa wale kumi na mmoja na kwa wengine wote. Hao waliowaambia ni Maria Magdalene, Yoana, na Maria mama yake Yakobo, pamoja na wanawake wengine waliokuwa pamoja nao. Lakini maneno yao yaliwaonekana kuwa kama upuuzi kwa wale mitume, wala hawakuyaamini. Lakini Petro aliondoka, akakimbilia kaburini. Alipochungulia ndani, akaona nguo za sanda peke yake; akarudi, akistaajabu moyoni mwake juu ya yaliyotukia.

SEHEMU YA PILI: TAFAKARI

KRISTO AMEFUFUKA KWELI ALELUYA!
Na, Pd. Nicas P Mrosso OFMCap

Katika sherehe ya Pasaka tunaadhimisha kilele cha mafumbo ya ukombozi wetu. Maadhimisho yetu yote ya sala, ya liturujia hupata maana kutokana na sikukuu ya Pasaka. Pasaka ndio utimilifu wa utume wa Yesu hapa duniani. Na ndio mwanzo mpya wa maisha ya Yesu ulimwenguni, na mwanzo mpya wa maisha ya ukombozi wa mwanadamu.

Pasaka ni Ushindi: Kristo ameshinda alleluia alleluia! Baada ya Ijumaa Kuu, Waliomuua Yesu walifikiri wamemaliza kila kitu, walifikiri wamemaliza habari za Yesu. Kumbe la! Hakika Ndio mwanzo mpya wa uwepo wa Yesu katika maisha ya kanisa, katika maisha yetu. Masaomo ya leo yanatuthibitishia hilo:

Somo la I: Kristo aliyeishi kati ya Wayahudi na akauwawa na Wayahudi ndiye anayeshi. Petro anatoa ushuhuda wa ufufuko wa Yesu. Kwamba Yesu mliyemuuwa, amefufuka na anaishi ni Mzima. Ufufuko wa Yesu unamfanya Petro aliyemkana Yesu kuwa mpya, na Kutangaza habari zake kwa ujasiri. Ufufuko wa Yesu usikuache kama jana, uskubali kubaki vile vile.

Somo la II: Kwa ufufuko wa Kristo, uhai wetu umefichwa ndani ya Kristo. Paulo anawaimarisha Wakolosai kwamba Masiah aliyesubiriwa na aliyeahidiwa, Mungu ametimiza ahadi hiyo katika Kristo. Ndiye Masiha aliyeaguliwa na kwa ufufuko ameketi Mkono wa kuume wa Mungu (Zab 1 1 0:1 ). Kristo ameketi Mkono wa Kuume na kuwafanya adui zake kuwa chini ya miguu yake. Adui wa kwanza aliyebatilishwa ni mauti.

Injili: Ushuhuda wa kwanza wa ufufuko wa Yesu ni kaburi wazi. Mariamu Magdalene anatudhihirishia hilo, asubuhi na mapema anakuta kaburi li wazi. Jiwe kuondolewa kaburini si kwa nguvu ya kawaida kwani waliliweka kubwa ili kuzuia wanafunzi wake wasije kumwiba. Uthibitisho wa pili ni ule wa Petro na mwanafunzi mwingine. Wanaona sanda na leso peke yake. Na uthibitisho mwingine ni Yesu kuwatokea wanafunzi wake na wafuasi wengine. Huu ni uthibitisho wa kihistoria ya kwamba Yesu amefufuka kweli.

Lakini swali ni Je, Ufufuko wa Yesu ni wa namna gani? Ni wa kibaologia, kama alivomfufu Larazo? Hapana! Wa lazaro uliitwa Resuscitation. Je Yesu ameingia katika hali ya mizimu/ghost? (kama baadhi ya tamaduni nyingi zinavyoamini mtu akifa anaingia kwa ulimwengu mizimu/spirits) Hapana!, licha ya kwamba anao uwezo wa kutokea katika hali ya roho.
Baba Mtakatifu Benedict wa XVI anasema: “Resurrection as something akin to a radical “evolutionary leap”, in which a new dimension of life emerges, a new dimension of human existence.” Maana yake ni mwanzo kabisa wa maisha mapya ya ufufuko. Yesu ameingia kwenye maisha ya umungu na umilele ambao nasi tunatarajia mwisho wa nyakati. Ambao hata sisi ambao hatukumshuhudia akiwa hapa duniani tunaweza kumwona. Ufufuko wa Yesu ni:
Maisha mapya: ufufuko wa Yesu ni kuingia katika maisha mapya, maisha ya umungu na ya umilele. Kuwekwa huru dhidi ya dhambi na mauti.
Ushindi: Kwanza ushindi dhidi ya mauti. Pia ni kushinda giza, kuwa watu wa mwanga, watu wa nuru kama tulivyoona liturujia ya mwanga jana usiku.
Kueneza habari njema ya Injili: Maria Magdalene anatufundisha hilo, amekuwa mmisionari wa kwanza wa habari njema ya matumaini.
Kushinda magumu: wala Jiwe, wala walinzi hawakuweza kushinda nguvu ya ufufuko. Kwa Kristo Mfufuka hakuna linaloshindikana, mwamini yeye/ Trust Him, Mkabidhi hilo jiwe linalokushinda.
Ufufuko wa Yesu ndio kiini cha imani yetu. Paulo anatuambia, Kristo asingefufuka kutoka wafu basi imani yetu ni bure (1 Kor 1 5:1 7) na hata kuhubiri kwetu kungekuwa bure (1 Kor 1 5:1 4).

Kristo amefufuka kweli Alleluia Alleluia!

Kurudi kwa Tafakari Zote