TUNAHITAJI KUSAHAU (TO UNLEARN) TULIYOJIFUNZA
~Admin
Kama ambavyo hatuwezi kupokea ikiwa mikono yetu imejaa, vivyo hivyo hatuwezi kujifunza ikiwa tayari tumeshafikia hitimisho la ambacho tungejifunza. Hitimisho "tulilojifunza" linatufanya kuwa na pendeleo (bias) kuhusu jambo lolote linalohusiana na swali ambalo tayari tumelihitimisha. Hii ndiyo sababu dini kubwa zote kwa namna moja au nyingine zinasema, “Usihukumu…†Kinachomaanishwa hapa ni kwamba tunapaswa "kusahau tuliyojifunza ili tuweze kujifunza upya," na ndiyo sababu tumetenga sehemu hii kwa ajili ya kufanya amali za taamuli (Contemplative Practices).
TAAMULI NA KUSAHAU TULIYOJIFUNZA KAMA KITU KILE KILE
Neno “contemplation†au taamuli limekuwa likitafsiriwa tofauti-tofauti kwa maana mbalimbali. Lakini, umewahi kusikia kuhusu "akili ya tamuli?" Kwa urahisi, akili ya taamuli ni uwezo ya kupokea na kuwa katika wakati uliopo, sasa hivi, bila kuhukumu, kuchambua, au kukosoa. Hii ni sawa kabisa na maana ya "kusahau tuliyojifunza."
Kuna hadithi kuhusu mwanafalsafa ninayempenda sana, Martin Buber (1878-1965), natumai inatoa somo lenye nguvu. Hadithi yenyewe kwa ufupi inasema:
Mfuasi mkubwa wa Buber aitwaye Friedman alimuuliza (Buber) kuhusu mtu aliyekuwa akimkosoa-kosoa (Buber). Friedman alidhani kwamba Buber alimwona mkosoaji wake, T. S. Eliot, kama mpinzani wake wa kiakili. Katika kitabu chake "Martin Buber and the Human Sciences," Friedman anaandika:
"Wakati nilipokutana na Buber kwa mara ya kwanza, aliniambia kuwa alikuwa amekutana na T. S. Eliot siku tano zilizopita. Nikamuuliza Buber, 'Hukubaliani na maoni ya Eliot?' Buber alinitazama na kusema, 'Ninapokutana na mtu, sichangamkii maoni yake; nachangamkia utu wake.' Nilichukulia hilo kama onyo, na kweli lilikuwa onyo. Nilikuwa nimewageuza hao wawili kuwa wapinzani wa kimantiki ndani ya mawazo yangu" (Friedman, 1996).
Kwahiyo, kusahau tuliyojifunza ni kujiondoa kutoka kwenye maarifa tuliyoyakusanya — yawe na faida au la — ili tuweze kukutana na uhalisia kama ulivyo, bila upendeleo wowote.
KWANINI "AMALI ZA TAAMULI" HAPA?
Lengo la sehemu hii si kuthibitisha jambo lolote kama mafundisho au kuanzisha hoja fulani, bali ni kufanya mazoezi au kwa neno jingine, "amali" zitakazotufanya tuweze kuishi kikamilifu katika wakati uliopo. Kwa njia hii, tutakapokuwa tumesahau tuliyojifunza, tutajipatia uwezo wa kujifunza vizuri kwakuwa huu ni uwanja zaidi wa wanaojifunza, kama unavyoitwa: Platform for Inspired Learners.
Kwa hivyo, tunasahau tuliyojifunza ili tujifunze upya, na sehemu hii ya AMALI ZA TAAMULI inatupa fursa ya "kujifunza kusahau tuliyojifunza."
Amali Njema!